AJALI YA MOTO YAUWA WATU WATATU, MAGOMI UCHUNGUZI UNAENDELEA, SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 1 December 2022

AJALI YA MOTO YAUWA WATU WATATU, MAGOMI UCHUNGUZI UNAENDELEA, SHINYANGA

Watoto watatu wa familia moja ya Bwana Mathayo Samson wamefariki dunia baada ya ajalinya moto uliowaka katika makazi ya famikia hiyo.



NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA


Tukio hilo la ajali limetokea leo Novemba 30, 2022 majira ya saa kumi na moja alfajiri katika mtaa wa Igomelo Kata ya Malunga Manispaa ya Kahama Mkoani smShinyanga.


Akithibitisha juu ya tukio la ajali ya moto, kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP, Janeth Magomi ambaye ameeleza juu ya tukio hilo huku akithibitisha vifo vya watu watatu waliofariki katika ajali hiyo ya moto.


“Leo tarehe 30 mwezi wa 11 ilikuwa majira ya saa kumi na moja asubuhi katika mtaa wa Igomelo kata ya Malunga Manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga Nyumba ya ndugu Mathayo Samson anaumri wa miaka 39 na mfanyabiashara Nyumba yake iliwaka moto na madhara yaliyosababisha ni vifo vya watu watatu”.amesema Kamanda Magomi Waliofariki katika ajali hiyo ni Dotto Juma mwenye umri wa Miaka 33 mkulima, Samson Mathayo mwenye umri wa Miaka 13 mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi ST. Antony of Padua pamoja na Joseph Samson mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi ST. Antony of Padua.


Kamanda Magomi amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokozi limefanikiwa kufika katika eneo la tukio Huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili kubainisha chanzo cha moto huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso