WANAUME WATAKIWA KUPIMA UKIMWI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 26 November 2022

WANAUME WATAKIWA KUPIMA UKIMWI

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, amewakumbusha wanaume wenzake kujenga tabia ya kwenda vituo vya kutolea huduma kupima Afya zao,ukiwemo UKIMWI ili kujitambua kama wapo salama na maambukizi ya virusi vinavyochangia ugonjwa huo.


Rai hiyo ameitoa alipokuwa anafungua maadhimisho ya wiki ya Ukimwi Duniani mwaka 2022,ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi uwanja wa Ilulu.


Katika ufunguzi huo,Ndemanga alikuwa anamwakilisha Mkuu wa Mkoa Zainabu Telak,ambapo amesema inashangaza kuona wanaume wamekuwa wazito kujitokeza kwenda kupima Afya,vikiwemo UKIMWI ili kujifahamu kama wapo salama na maambukizi ya VVU, badala yake wamekuwa nyuma kutekeleza hilo.


Amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016/2017,zinaonyesha kwamba kiwango cha upimaji kwa Mkoa wa Lindi,wakati wanawake waliojitokeza kupima walikuwa asilimia 55.9%.


Mkuu huyo wa Wilaya ya Lindi, amesema hali hiyo ni hatari sio tu kwa Mtu binafsi,Kaya bali kwa Taifa, kwani udhoofisha jitihada za serikali na wadau katika mapambano ya kutokomeza virus vya Ukimwi, huku akiwataka wananchi kuitumia wiki ya maadhimisho hayo,kujitokeza kupima afya zao bila malipo.


“Wanaume wenzangu tunakwama wapi,kila jambo tunazidiwa, kupima Afya tunazidiwa,idadi tunazidiwa ni wakati wa kujitafakari sasa”Amesema Shaibu Ndemanga.


Aidha ameongeza kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa na mtazamo hasi ya kutafasiri majibu ya vipimo vya virusi vya UKIMWI kutoka kwa wenza wao wanaokwenda vituo vya kutolea huduma kupima Afya zao, wakikutwa hawana maambukizi na wao wanadhani wapo salama sio.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso