WANANCHI 27 WANASAKWA NA POLISI HUKU VIONGOZI WANNE WA SERIKALI MKOANI TANGA WAKIKAMATWA NA POLISI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 14 November 2022

WANANCHI 27 WANASAKWA NA POLISI HUKU VIONGOZI WANNE WA SERIKALI MKOANI TANGA WAKIKAMATWA NA POLISI

Jeshi la Polisi limewakamata viongozi wanne wa Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga kwa tuhuma za kuuza ardhi ekari zaidi ya 500 na mbao 1,000 kinyume na utaratibu.

Viongozi hao wamekamatwa Jana Jumapili Novemba 13, 20 kufuatia agizo la Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba.


Mgumba ametoa agizo hilo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kwamsisi kusikiliza kero za wananchi ambapo amesema viongozi hao wametumia vibaya madaraka yao.


Pia, mkuu huyo wa mkoa ameagiza kukamatwa wananchi 27 ambao wapo kwenye orodha ya kudai kununua mashamba lakini hawako kihalali ila wametengenezwa na viongozi.


Viongozi waliokamatwa ni Mtendaji wa Kata ya Kwamsisi, Eric Chipindula, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwedikabu, Rajabu Makamba, Mtendaji wa Kijiji hicho Zahara Sempule na Ofisa Misitu wa wilaya Elinihaki Mdee.


"Takukuru fuatilieni hili suala lakini polisi kamateni hawa viongozi wote na wapelekwe ndani kwaajili ya mahojiano zaidi kwani wameshindwa kutumia vizuri nafasi zao", amesema Mkumba.

Viongozi wa vijiji hivyo wanatuhumiwa kwa nyakati tofauti kuuza zaidi ya ekari 500 za ardhi pamoja na kutumia vibaya madaraka yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso