WAGOMBEA UWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA WAWEKWA HADHARANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 14 November 2022

WAGOMBEA UWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA WAWEKWA HADHARANI


Na Mwandishi Wetu , SHINYANGA


KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, ametaja majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambayo yamepitishwa na Halmashauri kuu ya CCM Taifa.


Akizungumza kwa njia ya simu akitokea Dodoma, amewataja waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga kuwa ni Mabala Mlolwa ambaye anatetea kiti chake kwa awamu nyingine tena, Mwingine ni Costantine Mollo Nkuba na Eneza Onel Kanuya.


Nafasi ya ujumbe wa wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) waliopitishwa ni Gasper Hanson Kileo ambaye anatetea nafasi yake kwa mara nyingine, mwingine ni Nyachiro Maiga Magongo na Majuto Clement Manyilizu.

Chanzo:Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso