MWANAFUNZI ADAIWA KUBAKWA NA WATU WAWILI AKITOKA KWENYE MSIBA WA MAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 29 November 2022

MWANAFUNZI ADAIWA KUBAKWA NA WATU WAWILI AKITOKA KWENYE MSIBA WA MAMA

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Town(Jina lake limehifadhiwa) (17),mkazi wa Mwamala Kata ya Masekeleo Manispaa Shinyanga, Adaiwa kubakwa na watu wawili wasiofahamika akitoka kwenye msiba wa mama mzazi wa rafiki yake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital Shinyanga.


Tukio hilo limetokea Novamba 26, mwaka huu majira ya saa 4 usiku,katika mtaa wa Mapinduzi kata ya Ngokolo Manispaa na Mkoa Shinyanga.


Akieleza juu ya tukio hilo mlezi wa Binti huyo ambaye ni dada yake ,Ester Joseph amesema majira ya saa nane usiku aliamka kunywa maji sebuleni ndipo alipokuta mlango ukiwa wazi ambapo aliamua kwenda katika chumba anapo lala binti huyo,ndipo alipomkosa na kumkuta mjukuu wake akiwa peke yake chumbani.


Aidha Mlezi wa binti huyo,Ester Joseph ameeleza kuwa alimuuliza mjukuu wake dada kaenda wapi ndipo aliposema alimuacha akiwa anasuka sebleni ambapo alimwambia akimaliza atakuja kulala.


"Nilimpigia simu usiku ule nikamuuliza upo wapi akanambia nipo kwenye msiba wa rafiki yangu,nikamwambia rudi nyumbani sasa ivi,ila baada ya muda akatuma meseji nimetekwa,nakufa,mara gjafla nikamuona akiwa anashushwa na pikipiki akiwa na vijana wawili na kusema wamenibaka,nikamchukua na kwenda polisi kwaajili ya msaada"Amesema Ester.


Nae baba mzazi wa Binti huyo,Joseph Jinai,amesema kuwa taarifa hizo alizipata saa nane usiku ambapo alipigiwa simu mama mzazi wa binti huyo ambapo waliendelea kulala hadi asubuhi ili waende kuangalia kinachoendelea.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Mwamala,Musa Maswa amesema hana taarifa za tukio hilo huku akikiri kuwa muhanga huyo ni mkazi wa Mtaa wake.


Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP Janeth Magomi, Amesema kuwa hana taarifa zozote juu ya tukio hilo huku akiomba kupatiwa muda kwaajili ya kufanya upelelezi kwa OCD.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso