AFARIKI KWA SHOTI YA UMEME WA FENSI KATIKA KIWANDA CHA JIELONG,AKITOROSHA VYUMA ALIVYOIBA,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 14 November 2022

AFARIKI KWA SHOTI YA UMEME WA FENSI KATIKA KIWANDA CHA JIELONG,AKITOROSHA VYUMA ALIVYOIBA,SHINYANGA.

Kijana Mmoja Mfanyakazi wa kiwanda cha wachina cha Jielong kilichopo Nhelegani Manispaa na Mkoa Shinyanga,ambaye ni mkazi wa Katunda( 39), alifariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme wa fensi ya kiwanda hicho akiwa anajaribu kupitisha vyuma alivyokua ameiba akiwa kazini hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP Janeth Magomi

NA HALIMA KHOYA, HUHESO DIGITAL SHINYANGA

Kijana Mmoja Mfanyakazi wa kiwanda cha wachina cha Jielong kilichopo Nhelegani Manispaa na Mkoa Shinyanga,ambaye ni mkazi wa Katunda( 39), alifariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme wa fensi ya kiwanda hicho akiwa anajaribu kupitisha vyuma alivyokua ameiba akiwa kazini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja msaidizi,Sang Jeolong,ameeleza tukio hilo limetokea Novemba 8,2022 majira ya saa 3 usiku katika kiwanda hicho.

Meneja Msaidizi,Sang Jielong,Amesema kuwa kijana huyo alikuwa ni mfanyakazi bora wa kundi la wafanyakazi wa Kiwanda hicho huku akieleza kushangazwa na tukio alilokuwa amelifanya la kuiba,awali ya hapo alishawahi kupatiwa tuzo ya mfanyakazi bora Nchini China.

Aidha Amesema tukio la kuiba ni kwa mara ya kwanza kutokea katika kiwanda hicho ambapo baada amwbainisha baada ya kutokea tukio hilo alitoa taarifa Polisi kwaajili ya uchunguzi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza hatua za kiuchunguzi bado zinaendelea

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso