ZOEZI LA KUIAGA MIILI YA WATOTO WALIOUNGUA NA MOTO BUHANGIJA,RC MJEMA ASEMA SERIKALI IMETOA USAFIRI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 25 November 2022

ZOEZI LA KUIAGA MIILI YA WATOTO WALIOUNGUA NA MOTO BUHANGIJA,RC MJEMA ASEMA SERIKALI IMETOA USAFIRI.

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Sophia Mjema ametoa pole kwa wazazi wa watoto waliopoteza maisha katika ajali ya moto uliowaka kwenye moja ya Mabweni ya shule ya kulea watoto wenye uhitaji maalumu Buhangija lililokuwa na jumla ya watoto 32,waliookolewa 29 na waliofariki 3 lililotokea usiku wa Novemba 23 huku akiahidi kuwa serikali itasimamia zoezi zima la mazishi.

Umati uliofika kuaga Miili ya Marehemu ya Watoto waliofariki kwenye ajali ya Moto Buhangija Shinyanga.

NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Akizungumza katika zoezi la kuiaga miili ya watoto hao(Catherine Paulo ,Careen Mayenga na Nilium Limbu),ili kusafirishwa katika Makazi yao kwaajili ya kupelekwa katika Makazi yao ya kudumu leo novemba,24 mwaka huu lililofanyika katika hospitali ya Rufaa Mkoa Shinyanga.


Sophia Mjema,amesema vifo vya watoto hao ni mipango ya Mungu huku akibainisha kuwa Serikali bado inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo ili kubainisha kilichokuwa chanzo cha moto huo sambamba na kuwataka wazazi wakaze mioyo kwenye kipindi hichi kigumu.


“Najua ni ngumu kukubaliana na hili licha ya kuwepo kwa wazazi wanaoamini kuwa watoto wao ndio watakao wazika, hii ni mipango ya Mungu,serikali ipo pamoja na familia zote zilizopata msiba huu”Amesema Mjema.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa Shinyanga,Charles Ngelela,akitoa salam za pole kwa wafiwa amesema, chama cha mapinduzi kitakua pamoja na wafiwa wote sambamba na kubainisha kuwa kwa kila familia yenye msiba patakuwepo na Mwakilishi wa chama cha CCM.


Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa huo,wameeleza namna janga hilo lilivyo wagusa huku wakiiomba serikali kuweka Usimamizi na uangalizi mzuri katika shule za mabweni hali itakayosaidia kuondokana ajali za ghafla kwenye mashule hayo.

Wananchi wamejitokeza kwa wingi kuaga miili ya Marehemu ya Watoto walioungua kwenye ajali ya moto Buhangija Shinyanga


Majeneza yaliyo na Miili ya Watoto waliofariki kwenye ajali ya Moto Buhangija Shinyanga

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso