UTII, KATIBA NA UTUNZAJI WA SIRI KWA MAWAZIRI ZAMCHEFUA RAIS SAMIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 3 October 2022

UTII, KATIBA NA UTUNZAJI WA SIRI KWA MAWAZIRI ZAMCHEFUA RAIS SAMIA




Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri watatu huku akitoa angalizo kwa mambo matatu yanayoweza kumkwaza katika utekelezaji wa majukumu yao; utii katika maelekezo wanayopewa na Serikali, utunzaji wa siri za Serikali na utetezi wa katiba ya nchi bila kubagua upande.


Rais Samia anatoa maelekezo hayo leo Oktoba 3, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa viapo vya wateule hao baada ya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri kwa kuwahamisha wawili, kumuondoa mmoja na kumrejesha Angella Kairuki bungeni kisha kumteua kuwa waziri.


Rais Samia amemuapisha Kairuki ambaye alimteua kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania kisha kumteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) huku akimweka kando, Balozi Liberata Mulamula aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso