TANESCO KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATU 13 WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA SHIRIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 1 October 2022

TANESCO KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATU 13 WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA SHIRIKA

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashirikia watu 13 kwa tuhuma ya kuhujumu na kuharibu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania kati yao wakiwemo watumishi wawili na vishoka  wanne pamoja na  viongozi wa madhehebu ya dini wawili.


Na  Patrick Mabula , Kahama.



Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa wa Shinyanga  Janeth Magomi leo ijumaa  kwa waandishi wa habari katika kituo cha polisi cha wilaya ya Kahama alisema watu hao wanatuhumiwa kuhujumu miundombinu ya shirika ikiwemo kujiunganishia umeme kinyume cha utaratibu.

 

Kamanda Magomi alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na shirika la umeme Tanesco lilifanya oparesheni maalumu kwa lengo la kufichua vitendo vya kihalifu vinavyohusu uhujumu  wa miundombinu na liliweze kubaini na kuwakamata watu 13 kati ya hao 7 ni wateja wa shirika hilo.

 

Alisema watu hao wanatuhumiwa kujiunganishia umeme  kinyume cha sheria kwa kushirikiana na watumishi wa Tanesco wasikuwa waaminifu pamoja na vishoka wapatao na kundelea kutumia bila kulipia malipo yeyote.

 

Kamanda Magomi  alisema katika oparesheni hiyo  ilibainika watumishi wawili wasiokuwa wa aminifu kwa kushirikiana na waliodaiwa ni vishoka 4 walibainika kuhujumu miundombinu ya shirika kwa kuiba vifaa na kuwaunganishia wateja umeme bila kufaata taratibu kwa maslahi binafsi.

 

Alisema  imebainika kuwa jumla ya Transfoma 73 za umeme zimehujumiwa kwa kuibiwa vifaa mbalimbali na kusasabisha uharibifu na kulitia hasala shirika kwa zaidi ya shilingi milioni 10 kutokana hujuma hiyo iliyokuwa inafanywa na watuhumiwa pamoja na waliounganishiwa na kutumia umeme bule bila kulipa.

 

Kaimu meneja wa shirika la Tanesco wa wilaya ya Kahama, Mhandisi Tumaini Chonya  akifafanua kuhusu hujuma hiyo alisema baadhi ya wafanyakazi wasiokuwa waaminifu walikuwa wanaiba vifaa na kwenda kuwafungia umeme wateja yakiwemo makanisa ya madhehebu ya dini na kutumia umeme  bule.

 

Mhandisi Choya alisema hujuma iliyofanywa na watu hao ni kubwa sana kwa sababu wamelitia hasala shirika na kukwamisha jitihada za kupanua huduma kwa wateja ambapo ametoa wito kwa wananchi kuwa na moyo wa kutoa taarifa kwa Tanesco na jeshi la polisi juu ya vitendo vya hujuma ya miundo mbinu yake.

 

Aidha Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la umeme Tanesco linatoa wito kwa mwananchi yeyote anayeju kuwa amaunganishiwa umeme kwa njia zisizo halali na kwamba anatumia umeme bure bila kulipia bili kujisalimisha kwa ofisi ya Tanesco kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa ikiwemo kukamatwa.

 

Mwisho.


PICHA CHINI.



Vifaa mbalimbali vya shirika la umeme Tanesco zikiwemo mita  zilizokuwa zimefungwa kwenye nyumba za wateja kinyume cha utaratibu  vilivyokamatwa kwenye oparesheni iliyofanywa na kati ya Shirika na Jeshi la Poilisi mkoa wa Shinyanga kutokana na hujuma zilizokuwa zinafanywa na watumishi wasiokuwa waaminifu na vishoka wilayani Kahama , Picha na Patrick Mabula.


   

Kamamnda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga , Janeth Magomi akiongea na waandishi wa habari kuhusu oparesheni ya wahujumu wa miundombinu ya Tanesco na kukamata watu 13 wanaotuhumiwa kujihusisha na hujuma hiyo ikiwemo kunganishiwa umeme kinyume cha utaratibu ,Picha na Patrick Mabula.


Kamanda wa jeshi poilisi wa mkoa wa Shinyanga , Janeth Magomi akiwaonyesha Waandishi wa Habari vifaa vilivyokamatwa katika oparesheni iliyofanywa kwa ushirikiano na Tanesco kwa wanaofanya vitendo hivyo na kulisababishia shirika hasala ya zaidi ya shilingi milioni kumi.Picha na Patrick Mabula.


Kamanda wa Jeshi la polisi wa mkoa wa Shinyanga , Janeth Magomi akiwa na Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco wa wilaya ya Kahama Mhandisi Tumaini Chonya wakionyesha waandishi wa habari vifaa vilivyokamatwa kwenye oparesheni ya kuwakamata wanaofanya vitendo vya hujuma pamoja na kuunganishiwa umeme kinyume cha utaratibu hali iliyosababishia shirika hasala ya zaidi ya shilingi milioni 10.Picha na Patrick Mabula.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso