NAFASI YA KAZI NEW HOPE ORPHANAGE CENTER - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 2 October 2022

NAFASI YA KAZI NEW HOPE ORPHANAGE CENTER


Kituo cha kulelea watoto yatima cha New hope Orphange Center kilichopo Kahama Mwime Ilindi kinatangaza nafasi ya kazi ya mlezi na mwangalizi wa Watoto mwenye sifa kama ifuatavyo;

  • Awe wa kike mwenye umri kuanzia miaka 20 na kuendelea
  • Awe na Elimu ya Astashada (Certificate) Stashahada (Diploma) ya Ustawi wa Jamii (Social work) au Maendeleo ya jamii (Community Development)
  • Aweze kuishi kituoni ambapo atafanyia kazi
  • Awe na uwezo kutumia Kompyuta
  • Awe na uwezo kuzungumza na kuandika lugha ya kiingereza na kiswahili kwa ufasaha.
  • Awe na uwezo wa kutatua na kusaidia watoto hasa katika malezi na makuzi ya mtoto
  • Awe na wadhamini wawili wanaotambulika hasa wazazi na ndugu wa karibu
  • Awe Mkazi wa Kahama ambapo wamiliki wa kituo wataweza kufanya mawasiliano na familia kwa ukaribu
  • Awe mchapa kazi na anaweza kujituma
Andaa wasifu wako (CV) na picha moja passport size

Andika barua na tuma kwa 

Mkurugenzi Mtendaji
Kituo cha Kulelea Watoto yatima
New Hope Orphanage Center
S.L.P 145
Kahama

Au tuma kwa email newhopekahamatz@gmail.com 

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06 Octoba 2022 saa 12:00 jioni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso