BANDA LA KUKU LASABABISHA WATOTO WAWILI KUFARIKI KWA KUUNGUA NA MOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 31 October 2022

BANDA LA KUKU LASABABISHA WATOTO WAWILI KUFARIKI KWA KUUNGUA NA MOTO


Watoto wawili Meshack Ndimbwa (6) na Agrey Mgimba (2) wamefariki dunia na mmoja kulazwa baada ya kuungua na moto wakiwa wanacheza kwenye banda la kuku kijiji cha Lugarawa Wilayani Ludewa mkoani Njombe.


Akizungumza leo Oktoba 31, Mwenyekiti wa kijiji cha Lugarawa amesema tukio lilitokea Oktoba 29 majira ya asubuhi.


“Tukio hili lilitokea Jumamosi majira ya asubuhi, ambapo watoto hao walifariki wakati wakicheza ndani ya banda la kuku,” amesema Kayombo


Ameongeza kuwa chanzo cha banda kuungua ni moto uliopulizwa na upepo kutoka kwa jirani aliyekuwa anachoma mabua.


“Kuna kijana alikuwa anachoma mabua nyumbani kwake, nyumba yake inapakana na nyumba yenye vibanda vya kuku na nguruwe ambapo watoto wale walikuwa wakicheza, yeye baada ya kuchoma ule moto na kuona umetulia akaondoka.


“Ule moto ukapulizwa na upepo ukashika vile vibanda vya nyasi, sasa walipo kuwa ndani na kuona moto unakuja mtoto mmoja mkubwa alitoka na kukimbia wawili wakabaki ndani,


“Baadaye alirudi ili kuwaokoa wenzake, kwa bahati nzuri pale jiarani palikuwa na fundi anapaua nyumba baada ya kuona yule anarudi akaruka kwenda kumuokoa akamkamata lakini alikuwa amesha ungua,” amesema Kayombo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso