APIGWA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI - SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 6 October 2022

APIGWA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI - SHINYANGA

Mtu mmoja auawa na wananchi wenye hasira kali  Kata ya maganzo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoa Shinyanga kwa tuhuma za kuiba na kuvamia katika nyumba za wananchi  na kuwafanyika vitendo vya kikatili kwa kuwabaka baadhi ya  wanawake katika nyumba zao.



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP Janeth Magomi


NA HALIMA KHOYA-HUHESO DIGITAL- SHINYANGA

Tukio hilo la mauaji  limetokea leo Agosti 05 mwaka huu katika Kata ya Maganzo Halmashauri ya Wilaya Ya  Kishapu Mkoani Shinyanga majira ya saa 10 alfajiri.


Akisimuliwa Tukio hilo Mmoja wa wahanga wa kubakwa na mtu huyo Mary Dwashi, Amesema kuwa mtu huyo alimvamia katika nyumba yake wakati wa usiku na kumfanyia ukatili huo huku akiiomba Serikali kuweka ulinzi wa karibu kwa wananchi hali itakayolinda usalama kwa raia wote.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Maganzo,Castory Mkulima,amesema mtu huyo amekuwa akivamia katika nyumba za wananchi hao na kuwabaka wanawake hali iliyopelekea wananchi wenye hasira kali kumpinga kisha kumchoma moto mtu huyo.


“Nimeamka asubuhi nikakuta wananchi wamejaa katika eneo hilo nilipowauliza walisema wamemkuta mtu huyo ameanguka akiwa tayari kapigwa hivyo baada ya kugundua ni mwizi wakawa wamemchoma moto” Amesema Castory.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso