AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI MWENYE MIAKA 14 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 13 October 2022

AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI MWENYE MIAKA 14



Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga Linamshikilia Abubakar Saidi, mwenye miaka 64 Mkazi wa Ndembezi kwa tuhuma za kumbaka Mtoto wa Miaka 14 anayesoma kidato cha kwanza katika moja ya  Shule ya Sekondari iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.


NA HALIMA KHOYA, SHINYANGA.

Tukio hilo la kubaka limetokea oktoba 10 majira ya saa 8 mchana katika Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.


Akithibitisha juu ya tukio la ubakaji Kaimu Kamanda Jackson Mwakagonda,Amesema mtuhumiwa huyo ameshikiliwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 14 ambapo amesema kuwa, Mtuhumiwa huyo alimrubuni Mhanga kwa kumpatia elfu 10 kisha kumfanyia ukatili huo.


Pia Mwakagonda Ametoa wito kwa walimu wote kuwa, waweke ulinzi kwa kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi hao hali itakayosaidia kupunguza utoro katika shule zao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso