MGEJA AGOMEA MATOKEO,BAADA YA NGELELA KUTANGAZWA MSHINDI TENA UCHAGUZI WA MARUDIO NAFASI YA UENYEKITI CCM WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 19 October 2022

MGEJA AGOMEA MATOKEO,BAADA YA NGELELA KUTANGAZWA MSHINDI TENA UCHAGUZI WA MARUDIO NAFASI YA UENYEKITI CCM WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kimefanya uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Uenyekiti, pamoja Katibu wa Itikadi na Uenezi, mara baada ya uchaguzi wa awali kuingiwa na dosari.


Aliyeshinda Uenyekiti Edward Ngelela, akitoa neno baada ya Marudio ya matokeo ya uchaguzi wa Uenyekiti Wilaya Shinyanga

NA Halma Khoya, Huheso Digital SHINYANGA

Uchaguzi huo umefanyika Jana katika Uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga, ambapo uchaguzi wa awali ulifanyika Oktoba Mosi mwaka huu, na Edward Ngelela alitangazwa kushinda nafasi ya Uenyekiti, pamoja na Emmanuel Lukanda kushinda nafasi ya Uenezi.


Katika uchaguzi huo wa marudio, Edward Ngelela alitangazwa kushinda tena nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa kupata kura 741, akifuatiwa na Mwezetu Mgeja kura 157, Peter Kawiza kura 48, na Anna Ng’wagi kura 11.


Aidha, kwa upande wanafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Emmanuel Lukanda, alishinda tena nafasi hiyo kwa mara ya pili kwa kupata kura 120, akifuatiwa na Mohamed Hussein kura 10 na Rojas Samsoni kura Tatu.


Hata hivyo katika uchaguzi huo wa marudio Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti Mwezetu Mgeja, aligoma kusaini matokeo hayo kwa madai kuwa umegubikwa na figisu figisu.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmad Salum, amesema uchaguzi huo umekuwa wa demokrasia na haki, na amewaomba viongozi wawe na ushirikiano ili kuleta maendeleo ya ndani na nje ya chama.


"Uchaguzi umekuwa wa haki kwa kila mtu na hakuna ubishi wowote uliotokea na washindi wamepatikana, kinachofuata sasa ni kuchapa kazi kwa ushirikiano,”amesema Salum.


Peter Mashenzi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Ambaye ni Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Wilaya Shinyanga Vijijini Akisoma Matokeo baada ya Uchaguzi


Emmanuel Mabula Lukanda katibu mpya wa itikadi, siasa na uenezi wilaya ya Shinyanga vijijini akiwashukuru wajumbe


Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelala akizungumza baada ya kutangazwa mshindi

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso