WALIOGOMBEA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WAITWA NA CCM DODOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 2 September 2022

WALIOGOMBEA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WAITWA NA CCM DODOMA




Chama cha Mapinduzi kimewaita wanachama wake wote waliomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Bunge la Afrika Mashariki kufika kwenye kikao cha sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Jumla ya wanachama 155 wa chama hicho wameshachukua fomu za kuomba kuwania nafasi hizo, baada ya dirisha la uchukuaji fomu hizo kufunguliwa Agosti Mosi, 2022 na kufungwa rasmi Agost 10 Mwaka huu.


Taarifa ilitolewa leo Septemba 2 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka imewataka wateule hao kwenda na nyaraka zao zote muhimu zinazohusu sifa za kuwania nafasi hizo.


Shaka amesema pamoja na mambo mengine wagombea hao wameitwa kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki na uratibu wa vikao husika vya chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso