AJINYONGA KWA KUZIDIWA NA MADENI YA VIKOBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 15 September 2022

AJINYONGA KWA KUZIDIWA NA MADENI YA VIKOBA



Mkazi wa Kihesa Kilolo mkoani Iringa, Enea Mkimbo (55) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge kwa madai ya kuzongwa na madeni ya Vikoba.


Inadaiwa jana Septemba 13, 2022 wanakikundi wenzake walienda nyumbani kwake kudai madeni na ilipofika jioni akamuaga mumewe, Edward Sanga kuwa anakwenda nyumbani kwa mama yake mzazi na badala yake aliingia jikoni na kujitundika kitanzini hadi kufa.


Leo Septemba 14, Mwananchi imeshuhudia msiba wa Enea ukitengwa kwenye nyumba mbili kutokana na mvutano ulioibuka baina ya upande wa kike na kiume wakidai, hakulipiwa mahari.


Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha tukio hilo na kwamba, wanaendelea na upelelezi kuhusu madai ya Enea kujiua.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso