KATEKISTA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MIAKA NANE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 15 September 2022

KATEKISTA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MIAKA NANE



Jeshi la Polisi mkoani Geita, linamshikilia Athanas Rugambwa (62) mkazi wa Muganza wilayani Chato mkoani Geita kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka nane mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Katema.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Septemba 15, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amesema mtuhumiwa ni katekista na alikua akimfundisha mtoto huyo masomo ya dini.


Mwaibambe amesema mtuhumiwa huyo alimvizia mtoto akiwa kwenye mafundisho ya dini kanisani na kumuita ofisini kwake kisha kumbaka.


Mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa mahojiano na upelelezi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.


Pia, jeshi hilo linamshikilia Yusuph Ramadhani (31), mkazi wa Muungano wilayani Chato kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa miaka 17 wa shule ya msingi Chato na kumpa ujauzito.


Kwa mujibu wa kamanda polisi wanaendelea na uchunguzi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso