SPIKA TULIA AOMBA UFAFANUZI WA SAMAKI "CHANGUDOA" - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 25 September 2022

SPIKA TULIA AOMBA UFAFANUZI WA SAMAKI "CHANGUDOA"



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, juzi Septemba 23, 2022, Bungeni jijini Dodoma aliomba ufafanuzi wa aina ya samaki aitwaye changudoa, baada ya kuwa miongoni mwa samaki wanaopewa kipaumbele katika kukuza uchumi wa buluu.


Hatua hiyo ilijiri mara baada ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, kueleza mikakati ya wizara chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau wengine, kwa kusema imeweka mkakati na kutoa kipaumbele kwa dagaa, pweza, kambamiti, vibua, jodari, changudoa, unenepezaji wa kaa na ukuzaji wa lulu.


"Mheshimiwa Naibu Waziri, huyu anaitwa changudoa au changu mwenye madoa," aliuliza Spika wa Bunge


Ambapo Naibu Waziri Ulega alijibu, "Mh Spika, samaki huyu ana aina mbili tatu, katika mpango mkakati, yuko changu na yuko changudoa na changudoa ndiyo tumemkusudia katika mkakati wetu na si changu wa kawaida, na hili ni jina na linategemeana na mtamkaji,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso