SIMBA WAAMBULIA SARE DHIDI YA KMC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 7 September 2022

SIMBA WAAMBULIA SARE DHIDI YA KMC

 


VIGOGO, Simba SC wamelazimishwa sare ya 2-2 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.



Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake wapya, Mzambia Moses Phiri dakika ya tatu na mzawa, Habib Kyombo dakika ya 89, wakati ya KMC yamefungwa na Matheo Anthony dakika ya 47 na George Makang’a dakika ya 57.


Simba SC inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza ligi kwa wastani wa mabao dhidii ya mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi tatu.

Simba wakiongoza kipindi cha kwanza walitulia na kujiona wamefika japo kipindi cha pili ikawa kinyume na kujikuta wanajitumikisha ili angalau kupata sare.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso