MAYELE AWATETEMESHA ZALAN FC NA KUIPA YANGA POINTI TATU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 10 September 2022

MAYELE AWATETEMESHA ZALAN FC NA KUIPA YANGA POINTI TATU

 


BAADA ya dakika 45 za awali kutamatika katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku Zalan FC dhidi ya Yanga SC wakitoka bila bao. Kipindi cha pili kimeanza kwa Yanga SC kupiga mpira wa nguvu ambao umewawezesha kuimiminia Zalan FC kutoka nchini Sudan mvua ya mabao. 


Kocha wa Yanga, Prof. Nasreddine Nabi alipokwenda mapumziko aliwapa mbinu mpya za kuibuka na ushindi. Mayele dakika ya 47 kutupia bao ambalo liliwanyanyua mashabiki wa Yanga SC katika viti huku dakika ya 55 Feisal akitumbukiza bao la pili. Mabao yaliyofuata ni ya Mayele ambapo hadi dakika tisini zinatamatika katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga SC imejizolea alama tatu ikiwa na mabao manne kwa ushindi wa four G 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso