AKUTWA AMEJINYONGA KWA KAMBA KWENYE MTI WA MZAMBARAU - SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 13 September 2022

AKUTWA AMEJINYONGA KWA KAMBA KWENYE MTI WA MZAMBARAU - SHINYANGA

 

Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Hamis anyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 15-16 mkazi wa mtaa wa Iwelyangula kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba kwenye mti wa Mzambarau.


Tukio hilo limetokea leo Septemba 12, 2022, majira ya saa saba mchana ambapo kijana huyo mwenye umri chini ya miaka 18 amekutwa amejinyonga kwenye bustani ya matunda  kwenye mto unaotenganisha mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha na mtaa wa Iwelyangula Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.


Mwenyekiti wa mtaa wa Iwelyangula Robert Mnyeleshi ambaye ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa mfanyakazi wake akitokea Mkoa wa Kigoma na kwamba baada ya kumaliza kucheza mpira siku ya jana jioni hakurudi nyumbani.


“Jana alikuwepo kwenye saa kumi na mbili alikuwa anacheza mpira na vijana wenzake lakini baada ya kumaliza kucheza mpira hakurudi nyumbani tena, tukaanza kumtafuta usiku huo hatukuweza kumpata asubuhi tumeamkia kumtafuta ilipofika muda wa saa saba mchana wakaja vijana wawili walipita huko kwenye bustani wakaona mtu amening’inia juu ya mti waliponipa taarifa nikaenda kujiridhisha nikaona ni kweli ikabidi nipige simu polisi”,ameeleza.


“Kabila lake ni Mha mzaliwa wa Kigoma alikuja kwangu anatafuta kazi nikampa kazi ya kuchunga ng’ombe”, amesema  Mnyeleshi.


Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kupokea taarifa za kijana huyo na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.


“Nathibitisha kweli kupata taarifa hizo na jeshi la polisi limeshafika pale kwa ajili ya kuchukua mwili lakini hajaacha ujumbe wowote bado tupo kwenye upelelezi ili kubaini chanzo”,amesema Kamanda Magomi.

Chanzo - Misalaba blog,Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso