AJALI YAUA WATUMISHI TANESCO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 20 September 2022

AJALI YAUA WATUMISHI TANESCOGari lililokuwa na watumishi wa TANESCO


Watumishi watatu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) mkoa wa Manyara, wamefariki dunia katika ajali iliyotokea kwenye barabara ya Babati Singida.


Habari zaidi kutoka mkoani Manyara zinaeleza kuwa, watumishi hao wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakitumia aina ya Toyota Land Cruiser kugongwa na roli linalodaiwa kupata hitilafu katika mfumo wake wa breki.


Taarifa iliyotolewa na ofisi ya TANESCO mkoa wa Manyara imewataja watumishi waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Loren Materu, Emmanuel Thobias na Nassoro Mtime.


Majeruhi wengine watatu katika ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Mrara, kwa ajili ya kupatiwa matibabu

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso