RAIS SAMIA ASHIRIKI TAMASHA LA KIZIMKAZI,ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 3 September 2022

RAIS SAMIA ASHIRIKI TAMASHA LA KIZIMKAZI,ZANZIBAR

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa na vifaa vya matumizi ya aina mbalimbali katika mabanda ya Maonesho kwenye kilele cha   Tamasha hilo  la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022

   

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa mbalimbali vya Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar KMKM wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye Tamasha la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Kiazi Kikuu kilichochimbuliwa kwenye ardhi kavu na Wazee wa Jadi kutoka Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi katika Siku ya kilele cha Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022

    

  

Wataalam wa Jadi wa Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi wakionesha uwezo wa kufanya vitu mbalimbali wakati wa Sherehe za Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.

  

Wasanii wa Kikundi cha Zanzibar One wakitoa burudani kwenye Tamasha hilo la Kizimkazi lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.

   

   

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni mbalimbali wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi lillilofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso