RAILA ODINGA ASHINDWA KUHUDHURIA UAPISHO WA RAIS WILLIAM RUTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 13 September 2022

RAILA ODINGA ASHINDWA KUHUDHURIA UAPISHO WA RAIS WILLIAM RUTO

Kiongozi wa muungano wa Azimio La Umoja Raila Odinga jana alisema hatahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule William Ruto .


Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, Odinga alikiri kuwa Ruto alimwalika yeye binafsi kwenye hafla ya kuapishwa kwake lakini akasema hataheshimu mwaliko huo kwa vile yuko nje ya nchi na kwamba bado ana wasiwasi mkubwa kuhusu uchaguzi wa Agosti 9 ambao Ruto alitangazwa mshindi.


Odinga alikariri msimamo wake wa awali kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haikuendesha uchaguzi huru na wa haki.


Katika taarifa hiyo, Odinga aliendelea kushikilia kuwa anaamini kuwa uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi uliothibitisha kuchaguliwa kwa Ruto “haukuegemea ukweli na sheria, ingawa tuliukubali.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso