NILIKUWEKA PEMBENI KWA UTUNDU UTUNDU SASA UTAKUWA UMEKUA KAFANYE KAZI KWA UFANISI-RAIS SAMIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 1 August 2022

NILIKUWEKA PEMBENI KWA UTUNDU UTUNDU SASA UTAKUWA UMEKUA KAFANYE KAZI KWA UFANISI-RAIS SAMIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila atulize akili na kwenda kumsaidia kufanya kazi katika eneo alilompangia.


Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 1,2022 wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa aliowaapisha hivi karibuni.


"Mwanangu Chalamila mategemeo yangu umekua sasa, akili imetulia wewe ni mfanyakazi mzuri lakini mtundu mno, sasa nilikuacha nje kidogo kipindi hicho nimeamua kukurudisha naomba ukakue,ukue akili itulie uende ukafanye kazi ukanisaidie eneo ulilopangiwa na hii haina maana kwamba umemaliza ukikaa umekaa, nakuangalia kwa ukaribu sana",amesema Rais Samia.


Hivi karibuni Rais Samia alimteua Albert Chalamila kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera baada ya kutengua uteuzi wake akiwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Juni 11,2021.


"Ninapofanya teuzi hizi siangalii mambo mengine, Siangalii kabila, rangi ya mtu, anakotoka ninachoangalia ni sifa, uwezo, uaminifu wake kwa nchi na Serikali", amesema Rais Samia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso