MWANAMKE AKATWA MAPANGA NZEGA MUME WAKE AKIWA AMEENDA KUNUNUA ALIZETI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 11 August 2022

MWANAMKE AKATWA MAPANGA NZEGA MUME WAKE AKIWA AMEENDA KUNUNUA ALIZETIMkazi mmoja wa kitongoji cha Mwamakumbi (B) kikiji cha Nhabala Kata ya Nhalanga wilayani Nzega mkoani Tabora, Elizabeth Samson Ngudungi (35) ameuawa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu asiyejulikana.


NA PASCHAL MALULU-HUHESO DIGITAL


Tukio hilo limetokea Agosti 09, 2022 majira ya saa tatu usiku nyumbani kwa marehemu na wakati tukio hilo linatokea marehemu alikuwa nje ya nyumba yake akiwa amekaa.


Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Hamis Pasikali wamesema walipofika eneo la tukio baada ya kusikia kelele walikuta tukio hilo limefanyika na mtu alietekeleza amekimbia hivyo walichukua jukumu la kumpeleka mwanamke huyo hospitalini wakati akiwa amezimia kutokana na majeraha aliyapata.


Said Mkibuko ambae ni diwani wa Kata ya Kahama ya Nhalanga akizungumza kwa Simu na Mwandishi wa habari hii Paschal Malulu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema majira ya saa tano usiku alipokea simu majira ya saa tano usiku na kupewa taarifa ya tukio la mwanamke huyo Elizabeth Samson Ngudungi kukatwa mapanga.


Amesema kwa mujibu wa familia ya marehemu akiwemo mume wa marehemu  imesikitishwa na tukio hilo kukatwa mapanga kwa ndugu yao na haina wasiwasi na mtu yeyote kuhusika tukio hilo na wakati linatokea mume wake alikuwa amekwenda kununua zao la alizeti katika Kata ya Chambo halmashauri ya Ushetu huku ikiliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso