MWALIMU AUAWA KWA KUPIGWA MAWE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 13 August 2022

MWALIMU AUAWA KWA KUPIGWA MAWE

               Mfano wa mtu aliyelala barabarani


Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbaju Masasi mkoani Mtwara Mwanahawa Shaibu (50) ameuwa kwa kushambuliwa kwa mawe hadi kufa wakati akijaribu kumsaidia mtu aliyemkuta amelala barabarani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi (ACP) Nicodemus Katembo amesema mwalimu Mwanahawa kabla ya kukutwa na umauti alikuwa akitokea shuleni kwenda nyumbani Mbemba.


"Wakati akirudi nyumbani akiwa amepakiwa kwenye pikipiki alimkuta mtu akiwa amelala barabarani na aliposimama ili kujua mtu huyo amekutwa na matatizo gani hadi kufanya hivyo, ndipo aliposhambuliwa ghafla na mtu huyo kwa mawe bila sababu yoyote akaanguka na kupoteza maisha",amesema Kamanda Mbemba.


Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi.

chanzo: Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso