MOTO WA MGANGA WA KIENYEJI WA KUONDOA MIKOSI WAUA WATOTO-TABORA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 26 August 2022

MOTO WA MGANGA WA KIENYEJI WA KUONDOA MIKOSI WAUA WATOTO-TABORA




Watoto wanne wamefariki kwa kuungua moto uliowashwa na mganga wa kienyeji kwa lengo la kuondoa mkosi kwenye familia.


Watoto hao waliungua moto wakati wakigombania kutoka nje ya kibanda baada ya moto kuzidi.


Moto huo ulikuwa ukiwaka kuzunguka kibanda walichokuwemo pamoja na watu wengine ndani ya familia.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wanne wamefariki hadi sasa.


Amesema tayari mganga anayetuhumiwa kuhusika katika tukio hilo amekamatwa na upelelezi wake unaendelea."Ni kweli tuna taarifa ya tukio hilo na upelelezi wa tukio zima tunaendelea nao," amesema Kamanda Ambwao.


Kwa mujibu wa Diwani wa Kigwa, Bakari Kabata watoto waliofariki hawazidi umri wa miaka kumi na tano ambao ni wa familia moja.


Akielezea tukio hilo, Bakari Kabata amesema mwenyeji mwenye mji huo, alimuita mganga kwa mambo ya kimila, akimtaka kumuondolea mkosi kwenye nyumba yake na mganga huyo kusababisha maafa hayo.


Ameeleza kuwa mama wa familia ni miongoni mwa majeruhi saba ambao wamelezwa Hospitali ya Omulinga na ya Rufaa ya mkoa wa Tabora,Kitete.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso