MAAFISA WENYE VITAMBI JESHI LA UHAMIAJI KURUDISHWA VYUONI KUPATA MAFUNZO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 15 August 2022

MAAFISA WENYE VITAMBI JESHI LA UHAMIAJI KURUDISHWA VYUONI KUPATA MAFUNZO



Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza maofisa wa Jeshi la Uhamiaji waliopo kwenye vituo mbalimbali nchini, kurudi vyuoni kwa ajili ya kupatiwa kozi fupi za kuwajengea uwezo katika kazi zao.


Rais Samia ametoa agizo hilo leo Agosti 15, 2022 katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakati akizindua chuo cha mafunzo cha Jeshi la Uhamiaji cha Boma Kichakamiba ambacho kilianzishwa mwaka 2020.


Amesema Serikali yame imetoa fedha za kutosha kwa ajili ya mafunzo kwa maofisa kwa sababu wameona maofisa wa Tanzania wa vikosi vyote, kwa muda mrefu hawajapitia mafunzo hayo.


“Kwa hiyo tumetoa fedha nyingi ili maofisa warudi vyuoni, waje kupata tena mafunzo. Wapate refresher courses (kozi fupi). Wamesoma kozi za awali, wamemwagwa vituoni, wanafanya kazi zao lakini wanafanya kwa uzoefu. Kwa hiyo warudi hapa au vyuo vya majeshi mengine.


“Warudi wapate refresher courses, wapigwe msasa. Warudi tena kwenye vituo vyao ili wale wapya wakiingia wako vizuri, wale walioko vituoni wapigwe msasa ili wakiungana wote wanakuwa vizuri, jeshi linakuwa linafanya kazi vizuri,” amesisitiza Rais Samia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso