BREAKING NEWS : WILLIAM RUTO ASHINDA URAIS KENYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 15 August 2022

BREAKING NEWS : WILLIAM RUTO ASHINDA URAIS KENYATume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza makamu wa rais William Ruto kuwa rais mteule, kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, akimshinda mwanasiasa wa muda mrefu na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. 


NA TAIKILE TURO-HUHESO DIGITAL


Hata hivyo zoezi hilo limekumbwa na sintofahamu baada ya makamishna wanne wa tume ya IEBC kutangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa mchakato huo umekosa uwazi katika hatua za mwisho. 


Ruto amepata asilimia 50.49 ya kura dhidi ya asilimia 48.8 ya Odinga. 


Ruto amesema tume ya uchaguzi IEBC ni mashujaa na kwamba hakuna mshindi ispokuwa raia wa Kenya ambao wameinua kiwango cha siasa nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso