LESENI 470 ZA TANZANITE KUFUTWA HIVI KARIBUNI KWA KUDAIWA MAMILIONI YA FEDHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 13 August 2022

LESENI 470 ZA TANZANITE KUFUTWA HIVI KARIBUNI KWA KUDAIWA MAMILIONI YA FEDHA
Leseni za wamiliki 470 wa migodi ya madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara zipo mbioni kufutwa kutokana na kudaiwa Sh700 milioni za ada ya leseni za mwaka fedha wa 2021/22.


Ofisa madini mkazi wa Mirerani, Fabian Mshai ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau mbalimbali na wamiliki wa migodi na wachimbaji wa madini ya Tanzanite.


Mshai amesema kutokana na hali hiyo ofisi yake imetoa siku 30 kwa kila mdaiwa kufanya malipo hayo la sivyo watafutiwa leseni na kufikishwa mahakamani.


“Wale wote watakaoshindwa kulipa madeni yao watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria ya madini sura 123 pamoja na marekebisho yake,” amesema Mshai.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso