MENEJA RUWASA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MIRADI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 25 August 2022

MENEJA RUWASA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MIRADI

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, katikati ya mkutano na wananchi wa Kondoa Vijijini aliwaagiza polisi kumkamata na kumweka rumande Meneja wa RUWASA wa wilaya hiyo Mhandisi Falaura Kikusa, mara baada ya kubainika kushindwa kutekeleza mradi wowote tangu aingie ofisini kwa kipindi cha miaka minne.

Pichani ni waziri wa maji Jumaa  Aweso

Waziri Aweso amefikia uamuzi huo mara baada ya mbunge wa Kondoa Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji Dk.Ashatu Kijaji, kulalamikia utendaji kazi usioridhisha wa RUWASA katika eneo hilo na kusababisha wananchi kukosa maji safi na salama ya kutumia ,hali inayosababisha kuongezeka kwa magonjwa ya kuambukiza sambamba na kumsimamisha kazi Mhandisi huyo.


Katika hatua nyingine Mhe.Aweso na Dk. Kijaji wamewaonya nananchi kuacha kuchanganya siasa na vitu vya maendeleo vinavyofanywa na serikali.

Chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso