RAIS AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 25 August 2022

RAIS AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI

 

Rais Samia amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Mhe. Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.


Pili,amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Prof. Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.


Hayo ni kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa leo Agosti 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo ameeleza kuwa, uteuzi huo unaanza Agosti 23, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso