WANAFUNZI WENYE WATOTO WAOMBA BWENI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 14 July 2022

WANAFUNZI WENYE WATOTO WAOMBA BWENI



Baadhi ya wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatisha masomo kutokana na ujauzito wameomba kujengewa hosteli ambazo zitawasaidia kuishi na watoto wao.


Wamesema hosteli hizo zitawasaidia kuwa karibu na watoto wao kwa sababu kwa sasa wanakosa umakini wakiwa darasani kutokana na kuwa mabli nao.


Wametoa rai hiyo juzi wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dk Victoria Kwakwa alipofanya ziara katika Shule ya Msingi Turiani ya kufuatilia utekelezaji wa mradi wa kuwarejesha masomoni wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwamo ujauzito ambapo Shule hiyo ni mojawapo ya wanaotekeleza mradi huo.


Mmoja wa wanafunzi waliorejea masomoni baada ya kukatisha kwa miaka miwili kutokana na ujauzito, Joan Machange, alimuomba Dk Victoria waboreshewe miundombinu ya kujifunzia ili waondokane na mfumo wa kusoma nadharia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso