NYOTA WATANO WA KIKOSI CHA SIMBA WAACHWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 16 July 2022

NYOTA WATANO WA KIKOSI CHA SIMBA WAACHWA


Nyota watano wa kikosi cha Simba wameachwa Dar es salaam kwa ajili ya kuweza kutimiza majukumu yao kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stasr.

Wachezaji wa Simba.


Kikosi cha Simba Julai 14,2022 kilikwea pipa kueleka nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wale ambao watakuwa kwenye Timu ya Taifa hawatajumuishwa kwenye msafara.


“Tumeondoka na wachezaji wetu wote lakini wale ambao wataitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania hao watabaki kwa ajili ya maandalizi kisha wakikamilisha mechi watapata muda wa kujiunga na timu kambini,” amesema.


Wachezaji wa Simba ambao wameitwa katika timu ya taifa ni watano wanatarajiwa kuiingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu CHAN.


Ni Aishi Manula ambaye ni kipa namba moja, Mohamed Hussein na Kennedy Juma hawa ni mabeki na Mzamiru Yassin ambaye ni kiungo huku mshambuliaji akiwa ni Kibu Denis.

CHANZO:EATVNEWS

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso