KAMBI YA SIMBA SC MISRI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 16 July 2022

KAMBI YA SIMBA SC MISRI


Kikosi cha Simba kimefika salama nchini Misri baada ya safari yao kuanza jana Julai 14,2022 huku wakionyesha hoteli ambayo wamefikia kwaajili ya kambi ya siku 23 kwenye mji Ismailia nchini Misri


Kikosi cha Simba kilichoondoka nchini lJulai 14 mchana kwenda nchini Misri huku katika msafara wao walikuwepo wachezaji 19, benchi la ufundi pamoja na kiongozi mmoja ambaye ni Meneja wa habari na mawasiliano Ahmed Ally.


Wachezaji walioondoka walikuwepo, Shomari Kapombe, Ally Salim, Benno Kakolanya, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pape Sakho, Chris Mugalu, Augustine Okrah, Meddie Kagere, Jimson Mwanuke, Victor Akpan na Habibu Kyombo.


Wengine, Clatous Chama, John Bocco, Israel Mwenda, Joash Onyango, Henock Inonga na wengine wawili ambao hawakuonekana.


Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 Simba ilikwama kusepa na taji lolote na kuwafanya watani zao wa jadi kuweza kutwaa mataji yote matatu kuanzia Ngao ya Jamii,Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara.Kikosi cha Simba kimefika salama nchini Misri baada ya safari yao kuanza jana Julai 14,2022 huku wakionyesha hoteli ambayo wamefikia kwaajili ya kambi ya siku 23 kwenye mji Ismailia nchini Misri

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso