MWILI WA MWANAUME WAOKOTWA UKIELEA KWENYE BWAWA LA MAJI-MWANZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 28 July 2022

MWILI WA MWANAUME WAOKOTWA UKIELEA KWENYE BWAWA LA MAJI-MWANZA

Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 amekutwa amefariki katika bwawa la maji lililopo Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza huku akiwa na majeraha sehemu za jicho la kushoto


Diwani wa kata ya Buhongwa Joseph Kabadi amesema alipigiwa simu na wananchi na kuukuta mwili huo ukiwa unaelea kwenye bwawa hilo.


Yusuph Msalangi ni Mwenyekuti wa mtaa wa Nyaluhama lilipotokea tukio hilo ameesema bwawa hilo limekuwa likitumika kwa huduma ya maji kwa wananchi kutokana na changamoto ya maji huku akielezea matukio mengine ya vifo yaliyotokea katika bwawa hilo.


Mwili huo tayari umetolewa ndani ya bwawa hilo lakini mpaka EATV inaondoka katika eneo la tukio bado ulikuwa haujafahamika na chanzo cha tukio hilo hakijafahamika.

chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso