MIAKA 150 JERA KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA - TABORA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 30 July 2022

MIAKA 150 JERA KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA - TABORA



watu 5 wamehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela baada ya kupatikana na hatia unyan'ganyi wa kutumia silaha katika eneo la Urasa kata ya Mambali wilaya ya Nzega mkoani Tabora.


Na Lucas Raphael,Tabora


Akitoa hukumu hiyo jana Julai 29, 2022 hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya nzega mkoani Tabora mhere mwita alisema adhabu hiyo aliyoitoa iwe fundisho kwao na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo katika jamii.


Waliopatikanana hati ni Media Kafula,Masanja Nkuba,Mashiri Buyinga,Wiliumu Jeremia na Juma Sospeter mahakamani imeridhia kuwahukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela kwa kila mmoja.


Alisema kwamba kutokana na kosa walilolifanya washitakiwa hao na ushaidi uliotolewa mbele ya mahakama hiyo usioacha shaka yoyote mbale ya mahakama hiyo tukufu


Awali mawakili wa serikali kutoka ofisi ya mashtaka waliopo wilayani hapa nzega wakiongozwa na Jenifer Mandago waliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo jula 1 mwaka 2021 watu hao watano Media Kafula,Masanja Nkuba,Mashiri Buyinga,Wiliumu Jeremia na Juma Sospeter majira ya usiku wakiwa na silaha mbalimbali walivamia duka la Ufumba Kwirasa mkazi wa kitongoji cha urasa mambali na kumjeruhi kwa mapanga na kisha kumwibia zaidi ya shilingi laki saba pamoja na simu moja aina ya tekno.


Mawakili hao wa serikali waliendelea kusema kwamba kutokana na kosa hilo la jinai namba 9/2021 wanaiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwao na kwawatu wengine wenye nia na tabia kama hizo.


Hata hivyo mahakama hiyo ilitoa nafasi ya utetezi kwao kabla haijawatia hatiani ambapo waliomba kupunguziwa adhabu kwani wanafamilia zinazo wategemea.


Hakimu mhere mwita alitupilia mbali utetezo huo kwa kusema kwamba vijana mnatakiwa kutafuta fedha za alali na sio kumwanga damu kwa watu waliojitafutia mali kwa jasho na nyie kwenda kutumia nguvu kuzipora kwani hicho nikitendo cha kikatili kwa jamii ilijaa ustaharbu hivyo kifungo cha miaka 30 jela kwa kila mmoja wenu .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso