MCHUNGAJI AFARIKI AKIONGOZA IBADA YA MAZISHI-MTWARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 20 July 2022

MCHUNGAJI AFARIKI AKIONGOZA IBADA YA MAZISHI-MTWARA




Mchungaji wa Kanisa Katoliki kijiji cha Liputu, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Laurence Milanzi amefariki Dunia maeneo ya makaburini alipokuwa akishiriki mazishi ya mwanakijiji mwenzao aitwae Daudi Veno


Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mchingaji huyo alianguka ghafla wakati akiwaasa watu kutosusia misiba kwa mtu asiyehudhuria Nyumba za Ibada.


Kifo cha Mchungaji huyo kimetokea kwenye Kijiji hicho Julai 19 mwaka huu, saa 5:00 asubuhi kwenye eneo linalotumika mahususi kwa mazishi ya watu wanaofariki dunia.


Mwili wa Mchungaji huyo umehifadhiwa katika Hosptali ya Mission ya Ndanda, Wilaya ya Masasi ukisubiri taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kijiji hapo, baada ya kukamilika kwa taratibu zote.


Baadhi ya mashuhuda walioudhuria mazishi ya Daudi Veno, wameeleza kwamba, Mchungaji Milanzi amekutwa na umauti huo, alipokuwa anatoa sala na kuwasihi viongozi wenzake wa Dini kuacha tabia ya kutohudhuria mazishi kwa Binadamu mwenzao asiyeshiriki masuala ya Ibada.


Mchungaji Milanzi alisema kitendo cha kususa kumuombea marehemu kwa kuwa hakuwa anashiriki kwenye Nyumba za Ibada, Kanisani na misikitini ni kwenda kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu alivyoagiza mtu anapofariki ni muhimu akazikwa na sio kumuacha kwani uharibu hali ya hewa kutokana na harufu mbaya kutoka kwake.


“Baada ya kueleza hayo, tukamuona mwenzetu akidondoka chini kisha kupoteza fahamu” Walieleza Joseph Michael na Samwel Chindonga.


Aidha,mashuhuda hao wamesema kwamba baada ya Mchungaji huyo kudondoka chini walimchukuwa na kumkimbiza Hosptali ya Ndanda na kuelezwa na madaktari kuwa alishafariki.


Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi, na kuhifadhiwa chumba cha maiti (Mochwari) ukisubiri taratibu za mazishi.

Chanzo:EATV

2 comments:

  1. Ninamshukuru sana Dk dawn acuna, aliandika uchawi wa mapenzi ambao ulimrudisha mpenzi wangu wa zamani katika masaa 48, shukrani kwake, ikiwa una hali kama hiyo.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    Ikiwa unataka kuponya aina yoyote ya ugonjwa. Na wengine,
    Wasiliana naye yeye ndiye mtu sahihi wa kutatua tatizo hili.
    Barua pepe: { dawnacuna314@gmail.com }
    Whatsapp: +2348032246310

    ReplyDelete
  2. Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Post Top Ad

Pages

Huheso