DAVID KAFULILA AMSHUKURU MHE. RAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUMUUNGA MKONO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 29 July 2022

DAVID KAFULILA AMSHUKURU MHE. RAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUMUUNGA MKONO



Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.


Alhamisi Julai 28, 2022, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa ambapo amewateua wapya tisa, amewabadilisha vituo baadhi yao na wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi.


Katika mabadiliko hayo, wakuu wa mikoa tisa wameachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine, miongoni mwa walioachwa ni pamoja na Kafulila.


Wengine ni Ally Hapi (Mara), Robert Gabriel (Mwanza), Steven Kagaigai (Kilimanjaro), Charles Mbuge (Kagera), Wilbert Ibuge (Ruvuma), Marco Gaguti (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Rukwa), Binilith Mahenge (Singida).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso