BREAKNEWS: ALBERT CHALAMILA ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA KAGERA, MTAKA WA DODOMA APELEKWA NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 28 July 2022

BREAKNEWS: ALBERT CHALAMILA ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA KAGERA, MTAKA WA DODOMA APELEKWA NJOMBE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Cuthbert Sendiga na kumpeleka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.


Pia, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony John Mtaka na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Halima Omari Dendego, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.


Katika uteuzi huo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Babu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha.


Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt.Raphael Masunga Chegeni, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.


Pia Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Peter Joseph Serukamba, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

ORODHA YOTE HII HAPA





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso