BREAKINGNEWS: RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA MARA MPYA KABLA YA UAPISHO KESHO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 31 July 2022

BREAKINGNEWS: RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA MARA MPYA KABLA YA UAPISHO KESHO

 



Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mkuu wa Mkoa wa Mara mpya kabla ya uapisho wake kesho Jumatatu Agosti mosi 2022.

 

Taarifa ya kutoka ikulu ya Rais iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus imesema kuwa Mhe. Rais Samia amemteua Meja Jenerali Seleiman Mungiya Mzee kuwa mkuu wa mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni.

 

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Seleiman Mzee alikuwa kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP).



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso