BABA WA WATOTO WENYE UALBINO AKAMATWA AKIPANGA BEI KUWAUZA NA WANUNUZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 27 July 2022

BABA WA WATOTO WENYE UALBINO AKAMATWA AKIPANGA BEI KUWAUZA NA WANUNUZI



Baba ambaye anadaiwa kutaka kuwauza watoto wake watatu albino alikamatwa nchini Msumbiji wakati wakijadiliana kuhusu bei, polisi wamesema.


Mwanamume huyo, 39, na kaka yake, 34, walikamatwa katika jimbo la Tete magharibi.


Wamekanusha shtaka hilo, kwa mujibu wa polisi.


Watu wenye ualbino wameuawa nchini humo kwa ajili ya viungo vyao vya mwili vinavyotumika kwa matambiko.


Msemaji wa polisi Feliciano da Câmara alisema wanunuzi wawili pia wako chini ya ulinzi wa polisi.


Alisema watoto hao watatu wenye umri wa kati ya miaka 9 na 16 walichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kuzuiliwa huku mazungumzo ya bei yao yakiendelea.


‘’Uuzaji huo ulipaswa kufanywa kwa zaidi ya $39,100 (£32,400),’’ msemaji huyo wa polisi alisema.


‘’Tulichukua hatua na kuwapata watu hao wawili huko Angónia ambao walithibitisha mipango ya mpango huo,’’ aliongeza.

Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso