APIGA TENA SARAKASI MBUNGE WA MBULU VIJIJINI WAKATI WA TAMASHA LA MAJIMAJI SEREBUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 23 July 2022

APIGA TENA SARAKASI MBUNGE WA MBULU VIJIJINI WAKATI WA TAMASHA LA MAJIMAJI SEREBUKA

 

MBUNGE wa Mbulu Vijijini aliyetawala katika vichwa vya habari wakati wa mkutano wa bajeti uliomalizi jijini Dodoma, Flatei Gregory Massay amepiga sarakasi tena wakati wa uzinduzi wa msimu wa nane wa Tamasha la majimaji serebuka huko Songea mkoani Ruvuma.


Tamasha hilo limezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul ambaye amesema Serikali imekamilisha uchapishaji wa kitabu cha mwongozo wa maadili na sasa inaendelea na kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu maadili ya Mtanzania.




Amesema kuwa mchakato huo wa kukusanya maoni utakapokamilika serikali itakuja na mwongozo wa maadili ya Taifa ambao ni maelekezo yaliyotolewa na Rais, Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha vijana wa Kitanzania wakiwa katika maadili sahihi.





CHANZO: HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso