YANGA YAENDELEZA UBABE KWA KUICHAPA POLISI TANZANIA 2:0 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 23 June 2022

YANGA YAENDELEZA UBABE KWA KUICHAPA POLISI TANZANIA 2:0

 


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara NBC, Yanga imeendelea kutoa kichapo kwenye ligi baada ya leo kuichapa timu ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye uwanja la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Mchezo huo ambao ulikuwa wa 28 kwenye ligi ikiwa Yanga Sc ikicheza bila kupoteza mchezo wowote huku mshambuliaji wao Fiston Mayele akishindwa kupachika bao kwenye mchezo wa leo.


Mabao pekee ya Yanga yamewekwa kimyani na Feisal Salum "Fei Toto" pamoja na Chico Ushindi ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha kwanza na kuwafanya yanga kuibuka kidedea tena katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso