WATOTO 11,000 HUZALIWA NA SELIMUNDU (SICKLE CELL) KILA MWAKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 19 June 2022

WATOTO 11,000 HUZALIWA NA SELIMUNDU (SICKLE CELL) KILA MWAKA

 


Ikiwa leo Juni 19 Dunia inaadhimisha siku ya ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell), Jamii Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, imeaswa kujitokeza kupima afya zao ili kutambua endapo wana vina saba vya ugonjwa huo.


Na Duah Julius - Huheso Digital


Wito huo umetolewa na Mratibu wa Magonjwa yasiyo yakuambukiza Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Dokta Flora Mwinuka, amesema ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) sio wa kuambukizwa hivyo jamii ijitokeze kupima mapema ili kutambua hali zao za sasa.


Amesema Takwimu za Wizara ya Afya za 2021 zinaonyesha Nchini Tanzania Watoto 11,000 huzaliwa na Ugonjwa huo kila mwaka, ambao ni sawa na Watoto nane kati ya 1,000 wanaozaliwa, huku Kanda wa Ziwa Vicktoria ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi hapa nchini.


Aidha Dokta Flora ameongeza Manispaa ya Kahama inaadhimisha siku hii kwa na kwa kutoa Kliniki ya kupima na kutoa ushari zoezi litakalokuwa likifanyika kwa siku za Jumanne kila wiki katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.


Takwimu za Mwaka 2021 za Shirika la Afya (WHO) zinaonesha zaidi ya Watoto 1,000 Duniani huzaliwa wakiwa na Selimundu kila siku

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso