MKUU WA MKOA WA SHINYANGA SOFIA MJEMA ATEMBELEA KIKUNDI CHA KAHAMA HOPE GIVERS - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 17 June 2022

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA SOFIA MJEMA ATEMBELEA KIKUNDI CHA KAHAMA HOPE GIVERS





Mkuu wa Mkoa Shinyanga Sophia Mjema  amekipongeza  Kikundi cha   Kahama Hope Givers kwa kuanzisha Mama lishe na Baba Lishe Programme itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.


Na Naomi Kidunhu-Huheso Digital


Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kikundi  hicho  katika ofisi zao zilizopo maeneo ya Malunga wilayani kahama Mkoani Shinyanga, ambapo amesema  kuwa serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu itashirikiana nao ili wafikie malengo.


Mwenyekiti wa Kahama Hope Givers Ndg Simon Job Kassala  amemshukru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa  kuwatembelea  na kuahidi kuwasaidia  ili kuhakikisha lengo lao linafikiwa kwa aslimia kubwa


Kwa upande wao Baadhi ya Mama Lishe na Baba Lishe wametoa wito kwa jamii wajitokeze kwenye fursa mbalimbali zinazokuwa zinajitokeza ili kufikia malengo yao.


Kikundi cha   Kahama Hope Givers kimeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha na kuwakwamua Mama lishe na Baba Lishe itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sofia Mjema akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga wakiwa kwenye ofisi za Kahama Hope Givers

kushoto Katibu wa Kahama Hope Givers Ibrahim Makasy akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga pamoja na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sofia Mjema.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiwa anasikiliza mazungumzo ya mkuu wa Mkoa Sofia Mjema na kikundi cha Kahama Hope Givers

pichani ni Mwenyekiti wa Kahama Hope Givers akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sofia Mjema kwenye ofisi ya Kahama Hope Givers

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso