MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA MKUTANO WA UN WA BAHARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 27 June 2022

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA MKUTANO WA UN WA BAHARI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhifadhi wa Bahari na Rasilimali zake unaofanyika Lisbon nchini Uren leo tarehe 27 Juni 2022.Lengo la Mkutano huo ni kuhamasisha juhudi za Mataifa katika kufanikisha utekelezaji wa Lengo la 14 la Maendeleo Endelevu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhifadhi wa Bahari na Rasilimali zake unaofanyika Lisbon nchini Ureno


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali duniani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhifadhi wa Bahari na Rasilimali zake unaofanyika Lisbon nchini Ureno leo tarehe 27 Juni 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso