MABEHEWA SITA YA TRENI YAANGUKA MKOANI TABORA-MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 22 June 2022

MABEHEWA SITA YA TRENI YAANGUKA MKOANI TABORA-MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI

 


Mabehewa sita ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora mpaka Dar es salaam yameanguka leo Jumatano Juni 22,2022 katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi la polisi linaendelea kufuatilia kutokana na abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.


Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso