KARIBU NDONDO CUP YA CLOUDS FM 2022 KAHAMA USAJILI WAFUNGULIWA RASMI- BINGWA KUVUNA MAMILIONI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 27 June 2022

KARIBU NDONDO CUP YA CLOUDS FM 2022 KAHAMA USAJILI WAFUNGULIWA RASMI- BINGWA KUVUNA MAMILIONI

 



NA PASCHAL MALULU-HUHESO BLOG

 

Dirisha la usajili wa timu zitakazoshiriki mashindano ya Ndondo Cup ya Clouds FM 2022 limefunguliwa ambalo litadumu kwa muda wa siku saba (wiki moja) wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 

Akizungumza na wandishi wa habari za michezo katika mkutano wa kufungua zoezi hilo mwakilishi na mtangazaji wa kituo cha Clouds fm Yahya Mohamed (Mkazuzu) amesema Ndondo Cup katika wilaya ya Kahma itashirikisha jumla ya timu 16.

 

Amesema kila timu yenye nia ya kucheza michuano hiyo itapaswa kulipia kiasi cha shilingi laki mbili (200,000) katika chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kahama (KDFA) na usajili wa timu hizo unaanza rasmi Jumatatu Juni 27 hadi July 4, 2022.

 

Ameongeza kuwa michuano ya Ndondo Cup 2022 timu zote zinaruhusiwa kujisajili na idadi ikitimia ya timu 16 zoezi hilo litafungwa na mchakato wa upangaji wa ratiba na taratibu zingine zitafuata.

 

Nae mjumbe wa chama cha soka wilaya ya Kahama (KDFA), Julius Lugobi amewashukuru Clouds Media na Clouds fm kwa kuleta michuano hiyo katika wilaya ya Kahama kwani itakuwa fursa ya vijana kuonekana na timu mbalimbali nchini na kupata nafasi kwani Kahama kuna vijana wengi wenye vipaji lakini walikuwa wanakosa fursa ya kuonekana.

 

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Michael Kaijage amesema walituma maombi kwa uongozi wa Clouds Media kwa ajili ya kusogeza mkoani Shinyanga michuano hiyo ya Ndondo Cup na wanashukuru kukubaliwa kwa ombi lao.

 

Amesema mashindano hayo yanatarajiwa kuchezwa katika kipindi hiki cha mashindano makubwa nchini yamekwisha (Pre-season) na yatakwenda sambamba na uhamasishaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi ambapo fainali itachezwa siku mbili au tatu kabla ya zoezi hilo.

 

Hata hivyo michuano ya Ndondo Cup 2022 ya Clouds fm bingwa wa mashindano atazawadiwa milioni tano (5,000,000) na mshindi wa pili milioni tatu (3,000,000) huku yakiongozwa na kauli mbiu ya TWENDE PAMOJA JIANDAE KUHESABIWA.





 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso